Wadau nimukutana na maandishi haya mtandaoni, Shukrani kwa wadau Nelly kaminyoge na Atu Mwakalinga ambao wamenimuvuzishia. Nimeona sio mbaya na wengine wakayasoma na kuelimika. Ama kweli akina mama ni watu muhimu sana. endeeeleaaaa!!!!!
Acheni niwape heshima iliyotukuka wanawake woooooote;
IMAGINE:
ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa anakusamehe halafu anasahau!!!
UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia
UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI: Anakukaribisha, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.
UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!
CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza tokea hii; hana kinyongo!
UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruwale imenyooshwa
UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!
Na mengine meeeeengi sana wanafanyiwa hawa watu lakini WANASAMEHE, WANAVUMILIA! Ni watu muhimu
HIVI INGEKEWA WANAUME
TUNAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?
Kwa leo acheni tu niwape
heshima zao wanawake wote:
I SALUTE AND LOVE WOMEN