Mojawapo ya faida ya nmtandao ni kuelimishana. Rafiki yangu amenitumia taarifa hii ambayo kwangu naoina ni changamoto dhidi ya mfumo dume. Kwa kuwa blog hii inamuelekeo wa maudhui yaliyo katika taarifa hii, naumuvuzisha nikiamini itasaidia kwa njia moja ama nyingine kubadiri mtizamo ''wetu'' dhidi ya wanawake.
I SALUTE AND LOVE WOMEN
Kuna tukio naliona MAISHANI:Acheni niwape heshima iliyotukuka wanawake wooote Duniani;
IMAGINE:ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa anakusamehe halafu anasahau!!!
UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anakuchukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni kuchukiwa atachukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!
UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI(Umelewa): Anakukaribisha, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.
UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza tokea hii; hana kinyongo!
UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruwale imenyooshwa kama ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana kashasahau na kukusamehe!UNAMPA UJAUZITO(WENGINE PACHA): Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!Na mengine meeeeengi sana wanafanyiwa hawa viumbe lakini WANASAMEHE, WANAVUMILIA! Ni watu muhimu sana hawa watu maishani mwangu!
HIVI INGEKUWA WANAUME, WAKINA MIMI?
TUNAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?
Kwa leo na siku zote acheni tu niwape
heshima zao au zenu wanawake wote:
I SALUTE AND LOVE THEM WOMEN!