Friday, April 16, 2010

PASAKA NA UJASIRI WA WANAWAKE



NANI ALIYESEMA WANAWAKE NI VIUMBE DHAIFU?

NANI ALIYESEMA WANAWAKE NI WAOGA?

NANI ALIYESEMA WANAWAKE NI.....????????????


Ndugu zangu, mahubiri ya siku ya pasaka kanisani kwetu yaligusia suala muhimu sana,. Ni imani yangu kuwa mahubiri yale yalisaidia kuifungua mioyo ya wale wanaume na wanawake wanaodhani mwanamke ni kiumbe dhaifu. Kwa wale tulio Wakristo, kumbe pasaka ni uthibitisho na ukumbusho wa umuhimu na ujasiri wa wanawake duniani, Kwa maana nyingine , pasaka inabeba maudhui ya siku ya wanawake Duniani (8 machi).


Ni kwa nini nasema hivyo? Kwa kuwa wakati Yuda Eskarioti alimsaliti Yesu kwa kupokea rushwa na hatimaye kumwonesha Yesu kwa wauaji na Petro alimkataa Yesu mara tatu, wanawake walimlilia na kumfuata Yesu tangu wakati wa mateso hadi kufa kwake. Ni wanawake hao hao walioenda kabulini kumpaka mafuta Yesu wakakuta amekwishafufuka, ni wanawake hao hao ambao Yesu baada ya kufufuka alionekana kwao kwanza.


Ama huu ni ujasiri na upendo uliopindukia usiohitaji kiwango chochote cha elimu ya darasani kuutambua.

BRAVO Wanawake wote!!!!!!

No comments: