Reyhaneh Jabbari mwenye umri wa miaka 26 amehukumiwa kunyongwa baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mtu mmoja ambaye alifanya jaribio la kumbaka.
Taarifa iliyoripotiwa na CNN inasema mwanamke huyo amenyongwa katika gereza la Tehrain, Iran ambapo alikuwa amefungwa baada ya kutenda kosa hilo mwaka 2007 wakati huo akiwa na umri wa miaka 19.
Mwanamke huyo amekutwa na hatia hiyo kutokana na kosa la kumuua aliyekuwa mfanyakazi wa wizara ya ulinzi na usalama nchini Iran, Morteza Abdolali.
Shirika la kimataifa la haki za binadamu Amnesty International limelaani kitendo cha Iran kutoa hukumu hiyo, ambapo mbali na jitihada ya kampeni mbali mbali zilizofanywa ikiwemo zile za kwenye mitandao ya kijamii katika kuipinga hukumu hiyo kuonekana kutozaa matunda.
Taarifa kutoka nchini humo zinasema mahakama ilitoa hukumu hiyo baada ya kutojiridhisha na utetezi alioutoa mahakamani kwamba alitenda kosa hilo akiwa anajilinda.
Utafiti wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2011 unaonesha Iran ni moja ya nchi zinazoongoza kwa ukiukwaji wa haki za binadamu ambapo nchi hiyo ina wastani wa kutoa hukumu ya kunyongwa mtu 1 kila baada ya masaa 8
No comments:
Post a Comment