Tuesday, August 19, 2008

MADHARA YA VITA

Baadhi ya wakimbizi wa Kirundi katika kambi ya Mtabila
Ni dhahiri na ukweli usiopingika kuwa waathirika wakubwa wa vita ni watoto na wanawake. Wanawake wengi hujikuta wakibeba majukumu ya kulea familia pekee yao waume zao wakiwa aidha wamekufa au wamejichimbia kusikoeleweka kutafuta maisha. Hongera zao kwa wale wanaume ambao huamua kukabiliana na maisha na kubaki wakitunza familia zao katika kipindi hicho kigumu. Katika maisha haya ya ukimbizi watoto hujikuta wakipoteza utamaduni wao na kukosa malezi mazuri.Sote tunajua kuwa waanzishaji wa vita ni wanaume (mara nyingi) wakigombea vyeo vitakavyowawezesha kunufaisha matumbo yao kwa visingizio kedekede,mara eti wanadai demokrasia, mara wanataka kujitenga,mara wanataka hiki, kile, ili mradi tu kuhalalisha madhambi yao.Mifano ipo mingi mfano;Sidan,DRC,Burundi,Sri-Lanka,Chad n.k.
















































No comments: