Wanawake na watoto ndio waathirika wakubwa wa vita. Watoto hujikuta wakikosa mapenzi mazuri ya wazazi wao, wakipoteza muelekeo wa tamaduni zao kutokana na wazazi kuwa bize na mihangaiko ya kila siku wakijitafutia chochote na mbaya zaidi huathirika kisaikolojia na kujikuta wakijenga maisha ya utegemezi (kutokana na kuona wazazi wao wanavyopanga foleni kila mara kupokea misaada) na ubinafsi (kwani maisha ya kambini ni survival for the fittest). Katika vibanda hivyo vidogo mara nyingi faragha kwa wazazi huwa ngumu na hivyo kusababisha watoto wadogo kujifunza mambo makubwa kabla ya wakati wao....Hili ni tatizo na Tanzania tuna mifano mingi ya kujifunzia.
No comments:
Post a Comment