Friday, March 19, 2010

MFUMO DUME UNAANZIA HAPA


Tabia hii ya kugawa kuwa kazi fulani ni za wanawake na kazi fulani ni za wanaume ndiyo inayosababisha kazi ya kuutokomeza mfumo dume kuwa ngumu. Kwani huyo mtoto wa kiume angekuwa naye amebabe maji kuna tatizo gani? Kuna kila sababu ya kuamini kuwa inawezekana mtoto huyo wa kiume tayari aliishaambiwa kuwa kazi ya kuchota maji ni kazi ya wanawake- kazi ya kike. Tabia ya aina hii haifai katika jamii yetu, hebu tubadilike jamani.

No comments: